MTU mmoja mkazi wa Kijiji cha Igogwe kata ya
Bagamoyo wilayani Rungwe mkoani hapa amebadirika
ghafra na kuwa mlemavu wa ngozi (Arbino).
Akisimulia maajabu hayo mtu huyo Neema Masebo (26) alisema kuwa alipatwa na mkasa huo alipokwenda kijijini kwao kuwasalimia wazazi wake akitokea nyumbani kwake jijini Mbeya.
Neema
alisema kuwa Mama yake mzazi Tumaini Mlawa alipoona hali hiyo
alimkimbiza katika hospital ya Wilaya ya Rungwe Makandana kwa ajili ya
matibabu ambapo alilazwa siku 7 lakini hali yake ikaanza kubadirika
kuwa mbaya huku ngozi yake ikianza kuchubuka taratibu hadi alipobadilika
na kuwa mlemavu wa ngozi yaani (Albino)
Aliongeza kuwabaada ya madaktari kushindwa kuzuia hari hiyo isiendelee
alifika Mganga wa hospitali ya serikali ya Marekani, Dr, Jescar akiwa
katika ziara ya kikazi katika hospitali hiyo alimchukua vipimo na
kuvituma nchini kwake kwa uchunguzi zaidi lakini hakuletewa majibu, na
badala yake alipewa mafuta ya kuzuia mionzi ya jua na kuondoa vidonda,
aina ya AQUASPORT LOTION, ambayo yamemsaidia kutokuwa na vidonda,
Alisema
kuwa mara baada ya kupewa mafuta hayo alitoka hospital huku tayari
akiwa na ulemavu huo, ndipo alipotokea mama mmoja jirani yake ambaye
jina lake halikutajwa, aliyempeleka kwenye kanisa la maombi la Temple of
prayer for all nations church, la wilayani Kyela, ambako alifanyiwa
maombezi ikiwa ni pamoja na kupakwa mafuta ya upakona hatimaye hali yake imeanza kurejea taratibu.
Baadhi
ya wakazi wa kata ya Bagamoyo wilayani Rungwe wamelihusisha tukio hilo
na imani za kishirikina huku wakisema kuwa toka dunia hii ilipoanza
hawajawahi kuona tukio kama hilo la mtu wa kawaida kubadilika ghafra
kuwa na ulemavu wa ngozi yaani Arbino.
Mchungaji
wa kanisa hilo Nabii Charles Mkuvasa amekili kumpokea mgonjwa huyo
kanisani kwake na kwamba alipoletwa na mama huyo alikuwa na hali mbaya
lakini baada ya kumfanyia maombi na yeye kupokea uponyaji kutoka
kwa yesu kristo, nakusema kuwa hali yake sasa imeanza kurejea
taratibu na mungu yupo pamoja naye atarejea na kuwa kama zamani.
Na Eliud Ngondo, Rungwe
Subscribe to:
Post Comments (Atom)