SHULE YAPATA UWANJA WA MICHEZO


SHULE ya sekondari Mshikamano ya kata ya Igurusi wilayani Mbarali mkoani hapa imepata uwanja wa mpira wa miguu utakao isaidia shule hiyo kuchezea mchezo huo shuleni hapo.

Uwanja huo ni moja ya zawadi iliyotolewa na mgeni rasmi katika maafari ya kuwaaga wanafunzi wa kidato cha nne Septemba mwaka jana.

Akizungumza na NIPASHE mkuu wa shule hiyo, Mwl.  Mashaka Rashid alisema kuwa uwanja huo umekamilika kwa asilimia 95 ili kukamilika kabisa.

Alisema kuwa shule hiyo katika maafari ya kidato cha nne mgeni rasmi katika maafari hayo alikuwa ni mkuruigezi wa kampuni ya ujezi wa Bwawa la kuvunia maji linalojengwa katika kata ya Igurusi, ya Boymanda, Richard Mgaya ambae aliahidi kutoa visiki na kusawazisha eneo kwa ajili ya uwanja wa mpira.
Rashid alisema mkurugenzi huyo alipeleka shuleni hapo Katapila na kuanza kazi mara moja na kikamilisha ujenzi wa uwanja huo kwa kutoa visiki na kusawazisha na kuongeza kuwa sasa imebaki kuweka magori na kuanza kutumika.
Alisema ujenzi wa uwanja huo utaisaidia shule hiyo kuongeza uwezo katika michezo hasa katika Umiseta kwani wanafunzi wa shule hiyo watafanya mazoezi karibu na shule na kupunguza utoro mazoezini tofauti na hapo awali walikuwa wakifanya  hayomazoezi mbali na shule.
Aidha Mwl. Rashid alisema kuwa ujenzi wa uwanja huo umeghalimu jumla ya milioni 12 mpaka hapo ulipo fikia.
Kwa upandewake mkurugengezi wa kampuni ya Boymanda Richard Mgaya alisema kuwa kampuni yake kwa sababu ipo katika jamii na ni jukumu la kampuni kuisaidia jamii inayo wazuguka.
Kampuni hiyo inafanya ujenzi wa Bwawa la mradi wa umwagiliaji ambao upo katika kijiji cha Majenje kata ya Igurusi ni kijiji ilipo shule hiyo.