BAADHI ya miradi iliyoidhinishwa
na Baraza la Madiwani la Halmashauri ya Wilaya ya Mbarali mkoani Mbeya kwenye
bajeti ya mwaka huu wa fedha, bado utekelezaji wake haujakamilika licha ya kuwa
miradi hiyo haikuingizwa kwenye bajeti ya mwaka ujao wa fedha.
MKURUGENZI WILAYA MBARALI ADAM MGOYI KATIKA |
Hayo yamesemwa na Mkurugenzi wa
Halmashauri hiyo, Adam Mgoyi wakati wa kikao cha kawaida cha baraza la Madiwani
kilichokutana jana mjini Rujewa kwa ajili ya kupitisha makadilio ya bajeti ya
Halmashauri hiyo kwa ajili ya mwaka wa fedha wa 2013/2014
Alisema kuwa miradi hiyo bado
haijafa na kuwa itaendelea kutekelezwa kama ilivyokusudiwa kwa madai kuwa fungu lake lilishatengwa.
Mgoyi alilazimika kutoa ufafanuzi
huo baada ya baadhi ya madiwani kuanza kuilalamikia Serikali kuwa haitoi fedha za
miradi ambayo imeombewa fedha na Halmashauri hiyo kwa wakati na kusababisha
miradi hiyo kudolora.
Awali baadhi ya madiwani hao
walitoalionyesha wasiwasi wao juu ya miradi ambayo ilikuwa bado haijakamilika,
huku kwenye bajeti inayoandaliwa ikiwa haijaingizwa.
Kwenye malalamiko yao madiwani
hao walisema kuwa kuna maeneo
mengi ambayo miradi hayajatekelezeka kutokana na kukosa fedha za uendeshwaji katika
bajeti ya mwaka wa fedha unaomalizika, hali inayotia shaka kama miradi mipya
iliyoingizwa kwenye bajeti ya mwaka ujao itatekelezwa.
Baadhi ya miradi iliyotiwa shaka
na madiwani hao ni pamoja na ujenzi wa shule za msingi, Nyumba za walimu na
baadhi ya muindombinu ya barabara ambayo walidai kuwa bado haijatekelezeka.
Katika ufafanuzi wake Mgoyi alisisitiza kuwa miradi hiyo bado
inatambulika na kwamba hata kwenye vikao vijavyo itaendelea kuzungumzwa ili utekelezaji
wake uweze kuendelea na hatimaye kukamilika.
“Niwatoe hofu kuwa
miradi hiyo bado inatambulika na inao umuhimu mkubwa kwa maendeleo ya wanachi
wetu, hivyo hata kwenye vikao vijavyo itaendelea kujadiliwa ili tuweze
kuona namna ya umaliziaji wake hata kama kwenye bajeti mpya miradi hiyo haipo,”
alisema Mgoyi.
Kwa upande wake, Afisa Utumishi
wa Halmashauri hiyo Aswege Kaminyoge, alisema kuwa miradi mingi inaonekana kuwa
bado haijatekelezwa kutokana na serikali kutopeleka
fedha kwa halmashauri kwa muda muafaka hivyo kupelekea ucheleweshwaji wa
utekelezaji wa miradi hiyo.
Kaminyoge aliongeza kuwa iwapo fedha hizo zitapatikana hakuna
mradi ambao ulipitishwa utakaoshindwa kuutekelezwa kwa kuwa ni utekelezaji wa
miradi hiyo ni sehemu ya maendeleo katika halmashauri hiyo.