MAMLAKA YA MAJI SAFI NA MAJI TAKA YAANZISHA HUDUMA MPYA KWA WATEJA WAKE



MAMLAKA ya maji safi na maji taka mkoani Mbeya imeanza kutoa huduma mpya ya kuwaunganisha na mabomba ya maji taka kwa wateja wake kweye makazi yao kwa bei nafuu.

Hayo yamebainishwa na mkurugenzi wa mamlaka hiyo Eng. Simon Shauri wakati akizungumza na waandishi wa habari ofisini kwake mwishoni mwa wiki.

Huduma hiyo itatolewa gharama ya chini kwa wateja wake kwa kutoa mambomba ili kila mjeja aweze kutumia huduma hiyo mpya ya majitaka katika nyumba zao.

Alisema kwa kuzingatia kuwa ‘maji ni uhai na usafi wa mazingira ni utu’ mamlaka yake imedhamilia kuboresha huduma hiyo kwa kuhakikisha kuwa wateja ambao hawakuwa na huduma hiyo wananufaika zoezi hilo.

Eng. Shauri alisema kuwa mamlaka inaunganisha huduma kwa bei nafuu kwa kutoa mita bure na kuwa mita zipo za kutoa kwa zoezi hilo.

Aidha mkurugenzi huyo amewataka wakazi wanaoishi karibu na mabomba ya mfumo wa maji taka wajiunge, kwani gharama ni nafuu na kwamba mamlaka itatoa bure mabomba yenye urefu wa mita 30 kwa kila mteja.

“Kwa wale wanao ishi karibu na yalipo pita mabomba ya majitaka watapatahuduma hiyo kwa urahisi kwani sisis kama mamraka tutatoa mabomba ya kutosha urefu wa mita 30 kwa kila mteja na tumejipanga kutoa huduma hiyo,” alisema Eng. Shauri

Aliongeza kuwa mpaka sasa mkoa wa Mbeya unazaidi ya wateja 30,000 waliojiunga na huduma hiyo mpaka mpaka kufikia mwezi Disemba mwaka jana.