Serikali ya Marekani
inatarajiwa kutangaza zawadi ya hadi dola milioni 33 hivi leo kwa mtu
atakayetoa taarifa za wanachama wa ngazi za juu wa kundi la al-Shabaab nchini Somalia.
Hii itakuwa mara ya kwanza
kwa mpango huo kutangaza zawadi kwa wanachama wa al-Shabaab, kundi lenye
mafungamano na mtandao wa kigaidi wa al-Qaida na linalotuhumiwa kufanya
mashambulizi ya kigaidi katika nchi za Somalia,
Uganda na Kenya.
Mpango huo utatoa hadi dola
milioni 7 kwa taarifa kuhusiana na muasisi wa al-Shabaab, dola milioni 5 kwa wasaidizi
wake watatu na hadi dola milioni 3 kwa wanachama wengine wawili wa ngazi za juu
wa kundi hilo.
