Waziri wa Uchumi wa
Ujerumani, Phillip Rösler, yuko kwenye ziara ya siku mbili nchini Saudi Arabia,
kujadiliana na viongozi wa Ufalme huo wa Kiarabu matatizo ya kifedha ya kanda
ya euro na kuendeleza mafungamano ya kibiashara baina ya mataifa hayo mawili.
Rösler amekutana na Waziri wa
Fedha wa Saudi Arabia,
Ibrahim al-Assaf, ambaye amethibitisha ahadi ya euro bilioni 10 kwa Shirika la
Fedha wa Kimataifa IMF kusaidia kuutuliza uchumi wa dunia.
Rösler amesema Ujerumani
inataka kuwa na dhima kubwa katika mipango ya uwekezaji mkubwa katika ujenzi wa
nyumba, afya, uhandisi na nishati wa Saudi Arabia.
