MOROGAORO: MAGEREZA ZAZIDIWA NA WAHALIFU



MAGEREZA nchini zinakabiliwa na msongamano wa wahalifu kutokana na kuwapo watu 38,000 wakati magereza hayo yana uwezo wa kuchukua waharifu 29,522.

Hayo yamebainishwa mjini Morogoro na Kamishana Jenerali wa Magereza, Augustino Nanyaro, baada ya kuwavisha nishani ya Mwenge wa Uhuru Daraja la Nne maofisa na askari magereza 37 katika sherehe iliyofanyika katika viwanja vya gereza la Mtego wa Simba Kingorwila mkoani Morogoro.

Amesema kukosekana kwa magereza katika baadhi ya wilaya kunachangia kwa kiasi kikubwa msongamano huo ambapo wahalifu wake wanalazimika kuwekwa katika magereza za wilaya za jirani.