ARUSHA: BUNGE LA AFRIKA MASHARIKI LAPATA SPITA MWANAMKE



MAGRETH Nnziwa amechaguliwa kuwa Spika wa Bunge la Tatu la Afrika Mashariki (EALA) kwa kupata kura 33 huku aliyekuwa mpinzani wake, Dora Byamukama, akipata kura 12.

Wabunge hao wote wanatoka chama tawala nchini Uganda, (NRA) na Magreth anakuwa mwanamke wa kwanza kuongoza chombo hicho.

Uchaguzi huo umefanyika kwenye ukumbi wa Bunge hilo ulioko kwenye Kituo cha Kimataifa cha Mikutano cha jijini Arusha (AICC) na kuhudhuriwa na Katibu Mkuu wa EAC, Dk. Richard Sezibera, viongozi mbalimbali wa kiserikali kutoka nchi wanachama wakiwemo mawaziri pamoja na mjane wa Baba wa Taifa, Mama Maria Nyerere.