MBEYA: UPELEZI WAKANILIKA KESI YA MAKABURU (WASAUZI)



UPELELEZI wa kesi ya wawekezaji wa mashamba ya kapunga walioshitakiwa kwa kumwaga sumu katika mashamba ya wananchi umekamili na kesi yao kupangiwa siku ya kuanza kusikilizwa.

Kesi hiyo inayowakabili raia wa Afrika Kusini wawekezaji wa mashamba ya Kapunga Rice ya wilayani Mbarali, wakili wa serikali Lugano Mwakilasa, akiwa na mwenzake, amesema upelelezi wa kesi hiyo umekamilika na kuanza kusikilizwa hivi karibuni.

Hakimu mfawidhi wa mahakama ya hakimu mkazi ya Mbeya, Seif Kulita, amesema, kesi hiyo itatajwa tena tarehe 20 kwa ajiri ya kupangiwa siku ya kuanza kusikilizwa.