MBEYA: MTU MMOJA AKAMATWA NA BANGI (GANJA)






JESHI la polisi mkoani Mbeya linamshikilia mkazi wa  Maporomoko mji mdogo wa Tunduma wilayani Momba baada ya kukutwa na bangi zaidi ya kilo moja.

Kaimu kananda wa polisi Mkoani hapa barakael Masaki, amemtaja mtuhumiwa huyo kwa ni Emmanuel Simwawa (19), alikamatwa na askari wakiwa doria maeneo ya Maporomoka Tunduma akiwa na kilo moja na Gramu 10 za bangi.

Masaki amesema kuwa mtuhuniwa huyo alikuwa na bangi zikiwa katika mfuko wa Rambo akizisafirisha kundanazo nchi jirani ya Zambia, pia ameongeza kuwa mtuhumiwa amewekwa mahabusu wakati upelelezi ukiendelea.