CHAMA cha waendesha bajaji
Isanga mkoani hapa
Kimeitaka serikali kuruhusu
bajaji kufika katika maeneo mbalimbali
Mkoani hapa
Akizungumza na Rock Fm,
katibu wa umoja wa bajaji Bw Kenedy Kayange ameseama kuwa usafiri mkubwa
unaotumiwa na watu wengi Jijini hapa ni bajaji, hivyo ameitaka serikali
kuwaruhusu kufika katika maeneo mbalimbali ya jiji.
Bw Kenedy amesema kuwa
barabara zinazo tumiwa na bajaji ni chache hali inayopelekea kuwa na msongamano
mkubwa wa bajaji katika barabara hizo na kuwa chanzo cha ajali nyingi.
