KONGO: ONYO LATOLEWA KWA WAMAREKANI
Msemaji wa kundi la waasi la M23 katika Jamhuri ya Kidemopkrasi ya Kongo amelionya jeshi la Umoja wa mataifa nchini humo Monusco, kutoliunga mkono jeshi la taifa katika mapigano na waasi hao.
Msemaji huyo Kanali Kazarama Vianey ametahadharisha juu ya urukaji ndege katika maeneo yanayodhibitiwa na waasi wa M23 akisema zitadunguliwa.
Wakati huo huo, Waziri mkuu wa Congo Matata Ponyo amemaliza ziara yake katika eneo la Mashariki mwa nchi hiyo, akisisitiza kwamba jeshi la Congo litamaliza vita vinavyoendelea katika eneo hilo.
