RAIS wa Zanzibar, Dk. Ali Mohamed Shein amesema Serikali
itaendelea kuimarisha maslahi ya wafanyakazi huku akitoa mwito kwa
wafanyakazi kutimiza wajibu wao.
Dk. Shein ameyasema hayo jana katika hotuba aliyoitoa katika kilele cha Sikukuu ya Wafanyakazi Duniani (Mei Mosi), zilizofanyika katika Ukumbi wa Hoteli ya Bwawani mjini Unguja na kuhudhuriwa na wafanyakazi na viongozi mbalimbali kutoka sekta ya umma na sekta binafsi.
Katika hutoba yake hiyo, ameeleza kuwa kuanzia sasa Shirikisho la Vyama vya Wafanyakazi (ZATUC) lifanye jitihada ya kuwataka wafanyakazi watimize wajibu wao tena kwa juhudi zaidi wakiwa makazini.
Ameeleza kuwa imefika wakati Shirikisho hilo liwashajiishe, liwaelimishe na ikibidi kuwakemea watumishi wanaochelewa kufika kazini na kuondoka kabla ya wakati kwani huo si utaratibu wa kazi.
Aidha, Dk. Shein amesema kuwa katika muundo wa Serikali anayoiongoza, alianzisha Wizara mbili muhimu kwa lengo la kuimarisha usimamizi wa masuala ya kazi, kukuza ajira na kunyanyua hali ya maisha ya wafanyakazi na wananchi ambazo ni Wizara ya Kazi, Uwezeshaji Wananchi Kiuchumi na Ushirika pamoja na Wizara ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora.
Wafanyakazi wa Zanzibar kupitia Shirikisho la Vyama vya Wafanyakazi katika risala yao, walipongeza juhudi zinazochukuliwa na Serikali chini ya uongozi wa Dk. Shein huku wakieleza wasiwasi wao kwa kujitokeza vikundi vinavyohatarisha amani kwa kukashifu wananchi wenzao na viongozi kwa visingizio vya