Kiongozi
wa upinzani nchini Myanmar na mshindi wa tuzo ya amani ya Nobel Aung
San Suu Kyi anatazamiwa leo kupiga hatua ya kihistoria na kuchukua kiti
chake bungeni.
Awali, Suu Kyi na wenzake kutoka chama
cha kidemokrasia, walikuwa wamesusia bunge, wakipinga kiapo ambacho
kinawataka kuheshimu katiba yenye kulinda nafasi ya wanajeshi katika
siasa za Myanmar.
Ingawa wameacha msimamo huo, wabunge 36 wa
chama cha National League for Democracy wameapa kuendeleza mapambano ya
kubadilisha katiba.
Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Ban Ki-moon
amefanya mazungumzo ya kwanza ya ana kwa ana na Suu Kyi, na kumsifu kwa
kukubali mawazo ya wengine wakati Myanmar ikipiga hatua ya kwanza
kuelekea kwenye mfumo wa kidemokrasia.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)