China na Urusi zimepinga shinikizo linalowekwa na nchi za magharibi kwenye Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa, kuweka kitisho cha vikwazo kwa Sudan na Sudan Kusini ikiwa zitashindwa kukubali maagizo ya kusitisha mgogoro baina yao.
Shirika la Habari la Reuters, limeripoti kuwa wajumbe wa nchi tano wanachama wa kudumu wa baraza la usalama, na wa Afrika Kusini ambayo ni mwanachama wa muda, walikutana Jumatatu kwenye ubalozi wa Marekani kwenye Umoja wa Mataifa, kujaribu kupata muafaka juu ya mswada wa Marekani kuhusu Sudan mbili.
Mswada huo wa azimio, unatishia vikwazo zaidi vya kiuchumi na vya kiplomasia kwa nchi hizo.