MWANAFUNZI wa Darasa la kwanza katika Shule ya
Msingi Dovya, Lazack Maulid (7), mkazi wa Yombo Darajani amekufa baada
ya kusombwa na maji na kuzama wakati akiokoa ndala zake aina ya
‘yeboyebo’ zilizochukuliwa na maji.
Kamanda wa Polisi mkoa wa Temeke, David Misime amesema mwanafunzi huyo alisombwa juzi saa 7.00 mchana wakati akicheza na wenzake kwenye mkondo wa maji yaliyokuwa yakitiririka kwa kasi katika eneo la Yombo Darajani.
Amesema wakati wakiendelea na mchezo ndipo ndala moja ya mwanafunzi huyo ilichukuliwa na maji.
Amesema maji hayo yalimzidi mwanafunzi huyo na hatimaye kunywa maji mengi na kusombwa kisha kuzama na kufa papo hapo.

Misime
alisema kuwa mwili wa mtoto huyo uliopolewa na wananchi wa maeneo hayo
na umehifadhiwa katika Hospitali ya Temeke huku polisi wakiendelea na
upelelezi zaidi.