WAALIMU nchini washauriwa kujiendeleza
zaidi kielemu ili waweze kuweka juu taaluma yao ya ualimu.
Rai
hiyo imetolewa leo na Bi: Veronica Chamamu katika maafari ya pili ya kutimu
mafunzo ya ualimu katika chuo cha Moroviani cha Mkoani Mbeya.
Bi
Veronica amesema walimu wanatakiwa kuwa mfano wa kuigwa katika jamii kwani
watoto watakao kwenda kuwafundisha watakuwa
wakifuata yale yanayofanywa na waalimu wao hivyo amewaasa kuwa wawe kielelezo
bora.
Katika
mahafari hayo jumla ya wahitimu 222 wamehitimu mafunzo hayo ya ualimu katika
chuo hicho kinacho milikiwa na kanisa la Moroviani Tanzania.
Mmoja
wa wahitimu katika chuo hicho ambaye amezungumza na ROCK FM aliyejitambulisha
kwa jina la Raphaeli Danson amesema wamepata mafunzo mazuri na ya kutosha, kwa
sasa wako tayari kwa ajili ya kujenga taifa katika nyanja ya elimu.