UYOLE MBEYA: WAFANYA BIASHARA WALALANIKA MAISHA MAGUMU



WAFANYA biashara wa soko kuu la Uyole jijini Mbeya wamelalamikia na kupanda kwa bei za mazao ya vyakula na kusababisha ugumu wa maisha kuongezeka.


Wafanya biashara hao wamesema kuwa uchumi wa Tanzania ni mbovu kwani bidhaa zinapanda bei bila mpangilio jambo ambalo huchangia wananchi pamoja na wafanya biashara kuwa na maisha magumu.


Akizungumza na Rock Fm mfanyabiashara wasoko hilo Bi. Lilia Owenya amesema kuwa changamoto wanazozipata katika biashara zao ni pamoja na kupanda kwa bei  za mazao ikiwa ni pamoja na  mchele, maharage, mahindi na bidhaa zingine kama mchele.


Hata hivyo Bi.Owenya Ameendelea kueleza kuwa wafanyabiasha wengi wameshindwa kuendesha biashara zao kutoka na kutopata faida kutokana na biashara wanazozifanya.


Aidha ameiomba serikali iangalie swala hilo ili kuweza kuwanusuru wafanyabiashara, wakulima na wafanyakazi ili kuinua uchumi wa nchi.