Chifu Kiongozi wa Kabila la Kisafwa Bwana Roketi Mwanshinga(pichani kushoto )
akiongoza jopo la Machifu kuweka tambiko la kukemea vitendo
vinavyohusisha na Imani za kishirikiana katika Shule tatu za Msingi
katika Kata ya Itenzi na Mwalimu Mkuu wa Shule ya Msingi ya Tambukareli (pichani kulia) .
Machifu wakiingia katika Ofisi ya
Mwalimu Mkuu Shule ya Msingi ya Tambukarelikufanya tambiko la kukemea
vitendo viovu vinavohusishwa na Imani za kishirikina katika Shule tatu
za Msingi, zilizopo Kata ya Itenzi.
Machifu wakiingia katika madarasa na kufanya tambiko la kukemea vitendo
viovu vinavohusishwa na Imani za kishirikina katika Shule tatu za
Msingi, zilizopo Kata ya Itenzi.
Wanafunzi wa Shule ya Msingi Igombe
wakiwasikiliza Machifu licha ya mvua kubwa iliyokua ikiendelea kunyesha,
katika zoezi la tambiko la kukemea vitendo viovu vinavyohusishwa na
Imani za kishirikina.
Wananchi waliojitokeza kutoka Kata ya Itenzi katika zoezi la Machifu waliofika katani hapo kutambika kwa lengo la kukemea
vitendo viovu vinavyohusishwa na Imani za kishirikina.