WANGA WAKAMATWA (WIZARD) AKA WACHAWI



Msaidizi wa Mgana Mzungu Dokta Pondanga kutoka Kijiji cha Manienga Wilaya ya Mbrali Mkoni Mbeya akiteketeza matunguli kwa kutumia kuni na mafuta ya taa (picha ya kushoto). Mganga wa Jadi Mzungu Dokta Pondanga akiwa ameshika moja kati ya majini yaliyokuwa yakitumiwa kwenda kunyonya  damu za wananchi wa Mtaa wa Mwambenja, Kata ya Iganzo Jijini Mbeya.Habari na Ezekiel Kamanga, Mbeya
Mganga wa Jadi Mzungu Dokta Pondanga kutoka Kijiji cha Manienga, Wilaya ya Mbarali Mkoani Mbeya akiwa ameshika moja kati ya pembe iliyokuwa ikitumika kama usafiri na mchawi/wachawi wa Mtaa wa Mwambenja, Kata ya Iganzo Jijini Mbeya.
Mganga wa Jadi Mzungu Dokta Pondanga kutoka Kijiji cha Manienga, Wilaya ya Mbarali Mkoani Mbeya akionesha Pembe ambayo huuzwa zaidi ya shilingi 400,000 kwa ajili ya kusafiria mchawi/wachawi wa Mtaa wa Mwambenja, Kata ya Iganzo Jijini Mbeya. (Picha ya kushoto). Matunguli yakiwa yamekusanywa kabla ya kuteketezwa kwa moto(Picha ya kulia).


Askari akihakikisha Amani, usalama na ulinzi unaimarika eneo hilo. 
 .

Mganga wa Jadi Bwana Mzungu Dokta Pondanga (49) kutoka Kijiji cha Manienga, Wilaya ya Mbarali Mkoani Mbeya amewasili Kata ya Iganzo Jijini Mbeya kwa lengo la kuondoa matunguli na majini yanayodaiwa kuharibu amani katika kata hiyo.

Ujio wa Mganga huyo umetokana na ombi la wananchi na viongozi wa kata hiyo baada ya kuchoshwa na vitendo vya kishirikina vinavyofanywa katika kata hiyo, ikiwa ni pamoja na kufa kwa ng'ombe zaidi ya 14 kwa muda wa mwezi mmoja, watoto kuanguka mashuleni, pesa kutoweka katika mazingira ya kutatanisha na vinyeshi kutapakaa kwenye Ofisi za walimu.

Mganga huyo Pondanga amepata kibali kutoka Serikalini na katani na kuhakikisha hakuna uvunjifu wa amani ambapo Serikali imetoa Askari wawili kuhakikisha hali ya ulinzi na usalama katika zoezi hilo unahimarika.

Siku ya kwanza ya ujio wake Aprili 29 mwaka huu ameweza kuibua matunguli, majini na madawa mbalimbali katika kaya nne za balozi moja kati ya tano ambazo zitatembelewa na Mganga huyo, baada ya kuibuliwa kwa vitu hivyo katika nyumba hizo vilichomwa moto.

Baada ya kumaliza kazi hiyo ya kuibua na kuchoma, Mganga huyo alitoa somo kwa wachawi na wanaojihusisha na imani hizo kuacha mara moja kwani hazita wasaidia katika maendeleo kwani hata wao waisha yao ni duni, licha ya kununua kwa gharama kubwa ushirikina huo ambapo unadiawa hugharimu shilingi 400,000.

Aidha alienda mbali kwa kusema kuwa baadhi ya matunguli hayo hutumiwa na wachawi hao kusafiria angani matharani kutoka Mbeya umbali wa Kilometa 800, hutumia nusu saa huku wakitumia damu za watu kama petroli ndio maana hutokea vifo vya ghafla na wengine upungufu wa damu jijini hapa.

Kwa uapnde wao wananchi walimshukuru Mganga Pondanga kwa kuwaondolea adha hiyo ambapo baadhi yao wanaojihusisha na imani za kishirikina wamezikimbia nyumba zao na wengine kutupia matunguli mtoni.

Hata hivyo ameongeza kuwa kwa wale waliokimbia matunguli yao hayatafanya kazi na yatateketezwa huko huko walipo na zoezi hilo linaendela mpaka hivi sasa.