AL-QAEDA WAZIDI KUJIUA

Mwaka mmoja umepita toka kifo cha kiongozi wa al-Qaeda Osama bin Laden katika eneo lake la maficho Abbottabad, Pakstani.
Muathirika wa shambulio la kujitoa muhanga kwenye Jumba la Maonesho la Taifa la Somalia tarehe 4 Aprili akiwa amebebwa kwenye machela.. [Abdurashid Abdulle/AFP]    Muathirika wa shambulio la kujitoa muhanga kwenye Jumba la Maonesho la Taifa la Somalia tarehe 4 Aprili akiwa amebebwa kwenye machela.. [Abdurashid Abdulle/AFP]
Uongozi wa sasa wa al-Qaeda katika maeneo ya mpakani kati ya Afghanistani na Pakistani, yanayoongozwa na Ayman al-Zawahiri hauonekani kuwa katika hali nzuri kwa sasa kama ilivyokuwa chini ya bin Laden katika miaka michache iliyopita ya uhai wake: hali ya kuzingirwa na upotevu wa viongozi.
Hata hivyo, hii haimaanishi al-Qaeda wameshindwa kabisa. Asasi hii inavyoonekana bado ina nguvu ya kutoa mwito kwa washirika wake, ambao wamekuwa na matawi duniani kote. Jibu la hivi karibuni sana la wito huo zilikuwa harakati za Somalia, Harakat al-Shabaab al-Mujahideen.
Wakati al-Shabaab walipoungana na al-Qaeda ilipokelewa kama “mafanikio” na mkuu mpya wa asasi hii, al-Zawahiri, ukweli unabaki kuwa taratibu zilizopo za harakati hizo za silaha za Somalia zinaonekana kushuka chini kama washirika wengine wa al-Qaeda na vikundi vyenye silaha kabla yake, ambao tafsiri ya maovu na siasa kali ya mafundisho ya Kiislamu yaliwatenga watu na kuwapeleka katika kujiunga na vikosi vinavyopinga.

Al-Shabaab waogelea katika kupingana

Mauaji na ulipuaji mabomu unaofanywa na al-Shabaab yanatoa picha kuwa kundi hili linashauku ya kuogelea kupingana na hali ya sasa.
Badala ya operesheni hii kupata kuungwa mkono zaidi na watu, kunaleta matokeo kinyume, kama inavyoshuhudiwa ulipuaji bomu uliofanywa na al-Shabaab tarehe 4 Aprili huko Mogadishu, ambalo lilidaiwa kugharimu maisha ya raia wasio chini ya sita, wakiwemo maofisa wa michezo ambao hawahusiki katika mapambano yanayoendelea kati ya al-Shabaab na vikosi vya serikali vilivyorudishwa nyuma na walinda amani wa Umoja wa Afrika.
Ingawaje harakati hizi zilisababisha ulipuaji wa idadi kadhaa ya mabomu hapo nyuma ambayo yalidaiwa kugharimu maisha ya raia wengi, shambulio lake la hivi karibuni katikati ya mji huu mkuu limekuwa kitu cha kufikiria kwa sababu limetokea baada ya kundi hilo kuwa washirika rasmi wa al-Qaeda Februari mwaka huu. Hii inamaanisha kuwa operesheni za al-Shabaab sasa zinadhaminiwa na asasi hii.
Kwa mujibu wa ripoti za vyombo vya habari, shambulio hilo la kujitoa muhanga lilifanywa na mlipuaji bomu la kujitoa muhanga mwanamke ambaye alijilipua mwenyewe katika Jumba la Maonesho la Taifa huko Mogadishu, lililoua watu si chini ya sita wakiwemo Mwenyekiti wa Kamati ya Olimpiki wa Somalia, na Rais wa Shirikisho la Mpira wa Miguu wa Somalia. Al-Shabaab hasa walikuwa wakimlenga waziri mkuu Abdiweli Mohamed Ali wakati akijiandaa kutoa hotuba katika jumba hilo la maonesho—ambalo lilifunguliwa tena hivi karibuni kwa mara ya kwanza katika kipindi cha miaka 20—lakini hakujeruhiwa.
Zaidi ya hayo kwa upande wa majeruhi wa ulipuaji bomu wa Jumba la Maonesho la taifa, lilikuwa pia ni lenye maumivu yanayokatisha tamaa kuwa shambulio hilo limekuja wakati ambao mji mkuu wa Somalia unaonyesha dalili za kuwa maisha yamerudia hali ya kawaida baada ya miaka zaidi ya 20 ya mapigano kufuatia kuanguka kwa utawala wa Said Barre mwaka 1991.
Tangu al-Shabaab waondolewe kwa nguvu Mogadishu mwezi Agosti 2011, kujiamini kwa Wasomali kunaonekana kuongezeka, kwa kuwa na shule mpya, maduka na migahawa wakifungua milango na jitihada za ujenzi upya zinaonekana wazi katika mji mkuu ulioharibika.
Kwa kuongezea, safari ya kwanza ya ndege ya kimataifa ilizinduliwa mwezi Machi kwa safari mbili za ndege kwa wiki na Shirika la Ndege la Uturuki.
Kwa hali hiyo, mashambulizi ya al-Shabaab katika Jumba la Maonyesha la Taifa yanaweza kusababisha matokeo tofauti kuliko ilivyotarajiwa, kwa kuwa vitendo hivyo vinaweza kuongeza hasira za wakazi wa mji mkuu, wanaotafuta kuanza maisha mapya.
Hata wale wachache waliopo katika harakati za Kiislamu nchini Somalia wanaelewa operesheni hizi haziendi vizuri kwa wale wanaojitambulisha kama wanajihadi.
Sheikh Hassan Dahir Aweys, anayeongoza kikundi cha waasi wa kiislamu cha Hizbul Islam hadi kilipoungana na al-Shabaab mwaka 2010, hivi karibuni alieleza maoni hayo.
"Niliwaonya ndugu zetu wa jihadi katika kikundi cha al-Shabaab dhidi ya umwagaji damu ya wananchi wa Somalia Waislamu na kuua raia wasio na hatia kwa jina na Uislamu,” Aweys aliueleza mkutano wa wafuasi wake tarehe 30 Machi.
Ukosoaji wake ulitokea wakati mkanda wa video uliowekwa katika intaneti mwezi Machi na Omar Hammami, anayejulikana pia kama Abu Mansour al-Amriki, ambapo alisema anahofu na maisha yake kutoka kwa al-Shabaab, kikundi ambacho amejiunga nacho miaka michache iliyopita ili kutekeleza “jihadi”. Al-Amriki aliongea katika mkanda wa video wa mgogoro wa kinadharia kati yake na al-Shabaab, lakini haikuwa wazi kama mgogoro ulikuwa kuhusu uhalalishaji wa mauaji na umwagaji damu.
Ingawa al-Shabaab walijibu kwa kusema hawakuwa na dhamira ya kumuua al-Amriki na kwamba wameanzisha uchunguzi kuhusu tukio hilo, ripoti zilisambaa kupitia vyombo vya habari kwamba al-Amriki aliuawa na pengine kukatwa kichwa mikononi mwa kikundi kidogo cha al-Shabaab.
Wakati kifo chake bado hakijathibitishwa na taarifa zinazodai kwamba bado alikuwa hai na anazuiliwa nyumbani ziliripotiwa hivi karibuni, al-Shabaab bado hawajasema chochote kuhusu ripoti ya kifo chake.
Kushindwa kwa hatima ya al-Amriki, na mpasuko unaoripotiwa katika nyadhifa za kikundi, kunawasukuma wachambuzi wengi wa Kisomali kukitangaza kikundi kwamba kipo katika “hatua za mwisho za kufa.”

Kama ilivyo Iraki na Yemeni, ndivyo ilivyo Somalia

Uhalalishaji wa al-Shabaab siku zote wa mauaji yake na upigaji mabomu unaonyesha wanafuata njia hiyohiyo ambayo washirika wengine wa al-Qaeda wamekuwa wakifuata siku za nyuma, ambayo ilisababisha kusambaratishwa kwao baada ya msaada wa wananchi kwa kuwa shughuli zao zilipungua.
Mfano wa wazi wa tukio hilo ni vitendo vya al-Qaeda huko Iraki chini ya uongozi wa Abu Musab al-Zarqawi.
Operesheni za Al-Zarqawi zilisababisha mamia ya vifo katika mabomu yaliyopigwa hovyo na mauaji ya kutisha ambayo hatimaye yaliwavuta Wairaki wengi, pamoja na baadhi kutoka iliyoitwa wapinzani wenye silaha dhidi ya wageni na vikosi vya serikali ya Iraki, kujiweka mbali na al-Qaeda na kuunganisha jitihada za kuwaondoa.
Ripoti za hivi karibuni kutoka Yemeni zinaonyesha hasira kama hiyo ikieneza mgawanyiko wa wananchi wa Yemeni. Wayemeni hao wanavikataa vitendo vya al-Qaeda katika Peninsula ya Uarabuni na washirika wake, Ansar al-Sharia, ambayo inalenga katika utekelezaji wa ufafanuzi mkali wa Sharia, pamoja na kutumia adhabu ya hadd.
Kukataliwa huko hakuko kwa wananchi wa Yemeni tu, bali kumeanza kusambaa miongoni mwa wafuasi wa Ansar al-Sharia wanaokataa vitendo vya al-Qaeda vya vifo vya kiholela, kama inavyothibitishwa na mauaji ya hivi karibuni ya wafuasi saba wa Ansar al-Sharia ambao walikataa kubeba mabomu ya kujitoa muhanga yaliyozilenga kamati za umma za upinzani katika mji wa Lawder kwenye jimbo la Abyan.
Kukataa kwa wanachama hao kufanya mashambulizi ya kujitoa muhanga bila shaka ni maendeleo yanayoonesha mgawanyiko wa ndani unaoendelea wa kikundi cha Yemen na kunaashiria kuwa baadhi ya wanachama wameanza kurejewa na fahamu zao na pengine wameshawishika kuwa kupigana pamoja na al-Qaeda ni kufanya kosa.
Ukataaji kama huo wa watu dhidi ya vurugu kulitokea nchini Algeria katika miaka ya 1990 wakati mauaji yaliyokuwa yanafanywa na Kikundi cha Waislamu wenye Silaha (GIA) kilisababisha hasira kubwa za umma, na kuamua kuisaidia serikali kuu kupambana na wenye itikadi kali. Mauaji ya kikundi katika vijiji vya mbali yalisababisha watu wa vijiji hivyo kujitolea katika vikundi vya kujihami wenyewe vilivyopewa silaha na serikali, na kukifanya kikundi cha GIA kisiwe na uwezo wa kutembea kirahisi katika maeneo ya vijijini na kuvisaidia vikosi vya usalama kuwafukuza na kuwamaliza wanachama wa kikundi hicho.
Vurugu za kutumia silaha nchini Algeria zimepungua sana tangu kung’olewa kwa GIA, ingawa Kikundi cha Wasalafi kwa Ajili ya Mahubiri na Mapambano (GSPC), kikundi kilichojitenga na GIA, kinaendelea kutumia vurugu. Katika alama ya kuwa al-Qaeda wameshindwa kujifunza kutokana na makosa yao kuwa vurugu hazilipi, GSPC alijiunga na al-Qaeda na kuwa rasmi tawi la al-Qaeda Kaskazini ya Afrika chini ya jina la al-Qaeda katika Maghreb ya Kiislamu mwaka 2007.
Katika kuonesha hayo, ni wazi kuwa al-Qaeda na washirika wao wanahitaji kupitia upya mbinu yao ya kuendelea na operesheni za mauaji na kupiga mabomu ambayo yanawaathiri wananchi wasio na hatia. Al-Qaeda bila ya shaka wanaelewa kuwa kutoungwa kwao mkono na umma kumewafanya wawe kama samaki walio nje ya maji…wanasubiri kufa.
Hata Bin Laden, kabla ya kifo chake, inaripotiwa alifahamu kuwa kundi lake lilikuwa na tatizo la taswira kwa umma, hasa wakati vitendo vyao vilipokuwa vinatofautiana na njia za usalama zilizotumika katika harakati za mapinduzi ya nchi za Kiarabu.
Matendo ya karibuni katika Somalia na Yemen, hata hivyo, yanaonesha kuwa bado hawajajifunza somo la msingi kuwa vurugu hazina manufaa. Kwa hivyo, jaribio lolote hapo baadaye, “litawapa jina jipya” al-Qaeda la kuwajumuisha na washirika wao wa maeneo hayo, na bila shaka yataendelea kulipuka.