NEW YORK: VIKWAZI DHIDI YA SUDANI NA SUDAN KUSINI VYAJADILIWA
Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa limezungumzia azimio ambalo linaweza kuruhusu vikwazo dhidi ya Sudan na Sudan ya Kusini, ikiwa nchi hizo mbili hazitaitika matakwa ya Umoja wa Afrika na kumaliza vita vyao vya mpakani.
Umoja wa Afrika umezipa muda wa masaa 48 pande hizo mbili zisitishe uhasama, zianze mazungumzo katika kipindi cha wiki mbili zijazo na kufikia makubaliano ya amani miezi mitatu baadae.
Mswaada wa azimio umependekezwa na Marekani unaunga mkono matakwa ya Umoja wa Afrika na kuzitolea mwito pande hizo mbili zisitishe haraka uhasama wao na kuwarejesha nyumbani wanajeshi wao.
Mswaada huo unasema Baraza la Usalama litachunguza kama matakwa hayo yanatekelezwa na ikilazimika hatua ziada zitapitishwa.
Mazungumzo ya Baraza la Usalama yamefanyika katika wakati ambapo mjumbe maalum wa Marekani kwa Sudan mbili, Princeton Lyman, anazungumzia matumaini ya kumalizika mapigano hivi