Wafanyabiashara hao walidai kuwa
wanatoa ushuru mkubwa
ambapo biashara wanazozifanya
haziwalipi kutokana na
ushuru wanaotoa kwa kusafirisha
mazao kutoka shambani
hadi katika masoko
wanayofanyia biasharazao
Mmoja wa wawafanya biashara
aliyejitambulisha kwa jina la Vaileti Lailonga,
alisema viazi mviringo katika soko hilo wanachajiwa gunia
shilingi (100) jambo ambalo
huwagharimu kiasi kikubwa
Nae Bupe Masanja ambaye
ni mfanyabiashara wa
ndizi alisema kuwa
wakati mwingine ndizi
hazipatikani kutokana na
hali ya hewa
kuwa mbaya jambo
ambalo husababisha bei
za zao hilo
kuwa juu
Wafanyabiashara hao
wameiomba serikali kwa kushirikiana
na uongozi kupunguza
ushuru wa mazao
ili kuweza kuwasaidia
wafanyabiashara hao.