MSHITAKIWA na mmiliki wa mashamba ya kapunga jana alizua
tafulani na mfanyakazi mmoja wa mahakama kuu kanda ya Mbeya baada ya kubainika
akipiga picha jengo la mahama.
Tafulani hiyo ilitokea baada ya mfanyakazi huyo kumfuata
shitakiwa huyo ambaye ni raia wa Afrika Kusini na mmiliki wa mashamba ya
kapunga alibainika na mfanyakazi wa mahakama hiyo akipiga picha jingo la
mahakama hiyo.
Mfanyakazi huyo ambaye hakutaka jina lake litaje
alimfuata na kumnwambia haruhusiwi kupiga picha jingo la mahakama na kumtaka
afute picha alizopiga lakini Afrika kusini huyo alikataa na kumtishia
mfanyakazi huyo wa mahakama.
“Mzungu huyo amepiga picha asubuhi wakati anaingia
mahakamani hapo asubuhi na alipokuwa anafika akaanza kupigapicha jengo la
mahakama nikiwa na maafisa wengine wengi hapa nilimfuata na kumtaka afute picha
lakini alikataa na kunitishia kama ningechukua
kamera hiyo,” alisema mfanyakazi huyo.
Mzungu alinitishia baada ya kumfuata nikimtaka afute picha
alizozipiga katika maeneo ya mahakama na alipotaka kuchukua kamera alitishiwa
na mzungu huyo.
Baada ya kutoka mahakama hiyo ambayo mzungu huyo alikuwa na
kesi mfanyakazi wa mahaka alimfuata na kumwambia afute picha alizopiga
kiusalama ndipo lilipo anza timbwili lingine na mawakili wa wazungu hao ambao
walikuja kwa ajili ya kuwatetea katika kesi yao inayo wakabili ya kumwaga viwatilifu
katika mashamba ya wakulima.
Alifika wakili aliye fahamika kwa jina la Masumbuko Lamwei
na kuanza kumtetea mzungu huyo na kusema kuwa ni ruhusa kupiga picha mahakamani
na kuwa mbona waandishi wanawapiga picha wao wakiwa na wazungu mahakamani hapo.
“Nionyeshe sheria inayo kataza kupiga picha mahakama na mona
waandishi wanatupiga picha