KESI ya wawekezaji wa mashamba ya kapunga iliyopangwa
kuungurumishwa leo imeahirishwa kutokana na mtafiti aliyefaya utafiti wa
viwatirifu vilivyomwagwa mashambani kuwa bado hajapatiwa mwendesha mashitaka wa
serikali.
Mwendesha mashitaka wa
serikali, Lugano Mwakilasa amesema Matokeo ya utafiti wa huo ulifanywa na
mtafiti kumkuu wa kilimo makao makuu Arusha na hadisasa bado mwendesha
mashitaka wa serikali bado haja pewa ili kesi iendeleo.
Kesi hiyo ina wakabili
wawekezaji kutoka nchini Afrika Kusini wanamiriki kampuni ya inayojihusisha na
kulima mpunga katika mashamba ya Kapunga wilayani Mbarali.
Hii imekuwa ni mara ya pili
kuahirishwa kutokana na kesi hiyo
kusubiri taarifa za mkaguzi mkuu wa kilimo aliyefanya utafiti wa
kemikali zilizo mwagwa katika mashamba ya wakulima walio jirani na kampuni hiyo
ya Kapunga.
Mbele ya hakimu Seif Kulita mwendesha mashitaka wa upande
wa serikali, Lugano Mwakilasa amesema matokeo ya utafiti bado hawajaupokea na bado
haujatumwa na mkenia mkuu wa kilimo.
Awali mahahakama hiyo ilitoa
amri kwa mawakili wa serikali kuhakikisha ndani ya wiki mbili kukamilisha
upelelezi wa kesi hiyo ikiwa ni pamoja na kuyapata majibu ya utafiti wa
kemikali zilizo mwagwa mashambani.
Kesi hiyo inaendeshwa na
mawakili waserikali wakiongozwa na Lugano Mwakilasa na upande wa washitakiwa una
mawakili watatu wakiongozwa na Aley
Luchengula.
Kutokana na kuto
kamilika kwa upelelezi na kufikishwa kwa matokeo ya utafiti huo kuwafikia
mawakili wa serikali mapema na kesi hiyo imeahirishwa hadi Juni 4 mwakahuu
itakapo tajwa tena.