Picha ya kwanza Mwenyekiti
wa mtaa wa Ilolo Kati Ngambi Ngambi (Kushoto), akifuatiwa na Samson
Kibole (katikati) wakiwa na Mwenyekiti wa CHADEMA wilaya ya Mbeya Bwana
John Mwambigija na aliyekuwa Mwenyekiti wa Mtaa wa Ilemi Joseph James
Mbela, walipokuwa wakipokelewa rasmi kutokea Chama Cha Mapinduzi (CCM)
kwa kuachia nyadhifa zao katika Mkutano wa hadhara uliofanyika Mtaa wa
Ilolo Kati. Picha ya Pili Diwani wa Kata ya Mwakibete (CHADEMA) Bwana
Lucas Mwampiki akionesha kadi zilizopokelewa kwa wanachama wa CCM ambao
wamejiunga na CHADEMA.
Picha ya Tatu Mwenyekiti wa CHADEMA
wilaya ya Mbeya Bwana John Mwambigija na akimtambulisha rasmi aliyekuwa
Mwenyekiti wa Mtaa wa Ilemi Joseph James Mbela, mara baada ya kukihama
Chama Cha Mapinduzi (CCM) na Picha ya Nne Ngambi K Ngambi akionesha
rasmi kadi ya CCM na kumkabidhi Diwani wa Kata ya Sinde mheshimiwa
Fanuel Kyanula (CHADEMA) mwenye shati ya rangi nyeusi.
Wimbi
la Wenyeviti wa Mitaa kujuzulu kutoka Chama Cha Mapinduzi (CCM), na kuhamia
CHADEMA limeingia katika sura mpya, baada ya Mwenyekiti wa Mtaa wa Ilolo Kati
Bwana Ngambi K Ngambi naye kujiuzulu.
Tukio
hilo limetokea Aprili 24 mwaka huu katika
Mkutano wa hadhara uliofanyika katika mtaa huo na kuhudhuriwa na baadhi ya
madiwani wa CHADEMA jijini Mbeya wakiwemo madiwani wa Kata za Mwakibete, Forest, Sinde ambaye alikuwa Mwenyekiti wa Mkutano huo.
Akifungua
mkutano huo Diwani wa Kata ya Sinde Mheshimiwa Fanuel Kyanula, alitoa taarifa
ya maendeleo ya ujenzi wa Shule ya Sekondari ya Sinde ambapo kila mwananchi
alikuwa akichangia shilingi 3,000 badala ya shilingi 10,000 za awali.
Aidha
mchango huo umesaidia kumalizia kabisa ujenzi wa madarasa hayo, amewashukuru
wananchi kwa kuitikia wito wa kuchangia mchango huo bila usumbufu na
kipingamizi cochote.
Diwani
Kyanula akielezea matumizi ya mchango huo umeweza kukidhi kazi ya upigaji wa
sakafu na uwekaji wa nyaya za umeme, hatua hiyo ambayo Mkurugenzi wa
Halmashauri alitoa pongezi kwa na usimamizi mzuri hadi kufikia kukamilika kwa
ujenzi huo.
Naye
Diwani wa Kata ya Mwakibete Bwana Lucas Mwampiki amempongeza mwenyekiti huyo wa
mtaa Bwana Ngambi na kwamba ni kiongozi mchapa kazi, hodari na hivyo wao kwa
sasa wamempata Kamanda ambaye ataongoza mapambano dhidi ya ubadhilifu.
Kwa
upande wake Bwana Gambi amesema kujiunga kwake CHADEMA ni hiari yake na wala
hajalazimishwa na mtu bali ni kuchoshwa ba ukandamizaji ambavyo vilikuwa
vikifanywa na CCM naye kwa kuwaonea huruma wananchi aliokuwa akiwaongoza.
Katika
mkutano huo watu kadhaa walikabidha Kadi za CCM wakiwemo Rose Mwashilindi (50),
Atusekelege Asumbisye (52), ambaye alikuwa balozi wa mtaa huo na Samson
Mwakibole.
Katika
hadhara hiyo Mwenyekiti wa CHADEMA wilaya ya Mbeya Bwana John
Mwambigijaaliwapongeza waliohamia kwa hiari yao kujiunga na Chama hicho na kudai kina
watu makini ndio maana kimekua kikipata mafanikio siku hadi siku na kutamba
2015 wataichukua dola.
Kuhama
kwa Ngwambi aliyekuwa Mwenyekiti wa mtaa wa Ilemi ni pigo kubwa kwa CCM kwa
kipindi cha hivi karibuni kwani Mwenyekiti wa mtaa wa Ilemi Bwana James Joseph
Mbela naye alihamia CHADEMA akidia amechoshwa na ufisadi uliokithiri ndani ya
CCM.