WAUMINI wa kanisa katoriki parokia ya Nzovwe iliyopo katika
halmashauri ya jiji la Mbeya wiki iliyopita hawakuamini masikio yao, baada ya
tangazo lililosema kuwa Padre Joseph Roes atarejea jumla nchini kwao Ujerumani
ifikapo Mei 15 mwaka huu baada ya kulitumikia
kanisa kwa kipindi cha miaka 47.
Simanzi hiyo kwa wakristo wa Nzovwe ina tokana na ukweli
kwamba Padre huyo ambaye amefanya kazi parokiani hapo kwa kipindi cha miaka
zaidi ya 11 tokea alipo wasili kutoka jimboni Tabora mwaka 2000, sio tu amekuwa
kipenzi cha waumini wa parokia hiyo bali pia alikubalika kutokana na huduma za
kiroho alizokuwa akizitoa mahari hapo.
Padre Roes ambaye anatoka shirika la wamishonari wa Afrika
alizaliwa Februari, 18 mwaka 1936 katika mji wa Bottrop, uliopo nchini ujerumani,
akiwa motto wa pili kuzaliwa kati ya watoto nane wa Mzee Johann Roes na mama
Bernadienne Roes.
Baba yake Mzee Roes
alikuwa ni mfanyakazi wa shirika la reli nchini Ujerunani, ambako
alifanya kazi kwa kipindi cha miaka kama 25-30 kabla ya kustaafu.
Kabla ya kujiunga na shirika la reli mzee huyo alikuwa
anafanya kazi kama mtaalamu wa kuezeka vigae kwenye nyumba mbalimbali nchini humo, na alipostaafu kazi ya reli
mwaka 1968 ndipo alipo fanya kazi ya usafi kanisani na kwenye kumbi za kanisa hilo pamoja
na sakrastia.
Padre Joseph alianza masomo yake mwaka 1942 hapohapo Bottrop
mpaka mwaka 1950 alipo jiunga na seminari ndogo ya shirika la wamishonari wa
Afrika, mpaka mwaka 1958 alipo hitimu rasmi masomo yake ya sekondari.
Alisema kuwa Kuanzia mwaka 1958-59 alisomea masomo ya
Falsafa katika shirika lao hilohilo la wamishonari wa Afrika, na ilipo fika
mwaka 1959 -60 alisomea NOVISIAT, ambayo ni mambo ya kiroho ya kanisa ndani ya
kanisa hilo.
Mwaka 1960 mpaka 1964 Padre joseph alisomea somo la
Teolojia Nchini Uingereza akiwa bado
katika shirika lao la wamishonari wa Afrika.
Padre Joseph alisema kuwa ilipofika mwezi .......................................
KWA HABARI ZAIDI BOFYA HAPA utaona na picha