MTENDAJI ASHINIKIZWA KUJIUZURU NA WANANCHI




WANANCHI wa kata ya Sangambi wilayani Chunya wamemshinikiza mtendaji wa kata ya hiyo kujiuzuru wadhifa wake kutokana na kuchangisha michango isiyo halali na kushindwa kufika katika mikutano zaidi ya mitatu.

Akizungumza na ROCK FM Bw. Junjulu Mhewa amesema mtendaji wa kata hiyoBw. Ndomba anatuhumiwa na wananchi wa kata hiyo kwa kuwachangisha wafugaji wa kata ya Sangambi michango ya ujenzi wa vyumba vya madarasa katika shule ya sekondari Charangwa lakini stakabadhi za malipo ya mchangohuo zikionyesha ni malipo ya kuchangia ujenzi wa shule ya sekondali Ibaba iliyopo wilayani Ieje.
 

BW Mhewa ameongeza kuwa pamoja na kuwepo kwa mkanganyiko wa stakabadhi hizo ziliendelea kutumika bila tahadhali yoyote ambapo wafugaji hao waliamua kuunda kamati ya uchunguzi wa swala hilo.
 
Hata hivyo kamati ilishindwa kupata ufumbuzi wa madai hayo hali iliyo pelekea kuitisha mkutano ambao umefanyika katika kata hiyo lakini mtendaji hakuweza kuuzulia pamoja na kwamba alikuwa na taarifa za kufanyika kwa mkutano.