MKULIMA ALAWITI



MKULIMA na mkazi wa Nunge mjini Morogoro, Juma Rashidi (55) anashikiliwa na Polisi mkoani Morogoro kwa tuhuma za kumlawiti mtoto wa miaka 14.

Kamanda wa Polisi mkoani Morogoro, Adolphina Chialo amesema kuwa Rashidi anatuhumiwa kufanya kosa hilo Aprili 22 mwaka huu saa 4 usiku katika Mtaa wa Karume Manispaa ya Morogoro.

Amesema Rashidi anatuhumiwa kumlawiti mtoto huyo katika uchochoro uliopo kwenye eneo hilo la Karume na atafikishwa mahakamani upelelezi utakapokamilika.