MWENYEKITI wa kamati ya wakuu
wa shule katika halmashauri ya Wilaya ya Mbeya Bw.Meshack Mlawa ameitaka jamii
kuwekeza nguvu kubwa kwenye elimu badala ya matamasha na harusi.
Ameyasema hayo hivi karibuni
ofisini kwake alipokuwa akizungumzia changamoto mbalimbali zinazojitokeza
kwenye harakati za kukuza kiwango cha elimu nchini,alipo kuwa akizungumza na
waandishi wa habari.
Ameogeza kuwa jamii
imeelekeza sana
nguvu kubwa kwenye matamasha na harusi badala ya kuelekeza kwenye
elimu ili kuandaa taifa lenye watu wasomi ambao wataweza kuongeza
nguvu katika uchumi wa nchi.
Mwenyekiti huyo pia amewataka
wazazi na walezi kutoa ushirikiano kwa walimu kufuatilia maendeleo ya
watoto wao wawapo shuleni badala ya kuwaachia jukumu hilo walimu pekee.
Mlawa amesema, mkoa wa
Mbeya umekuwa ukipata sifa za kushika nafasi za juu kielimu hapa nchini
kutokana na juhudi za Halmashauri hiyo ambayo ina shule nyingi zinazo fanya
vizuri katika elimu kitaifa.