WANANCHI wa Kijiji cha Ijumbi, Kata ya Ruiwa
Wilaya ya Mbarali Mkoani Mbeya, wamemuomba Mkuu wa Mkoa Bwana Abbas Kandoro
kuingilia kati mgogoro baina ya pande mbili zinazopingana kati ya Diwani na
Afisa Mtendaji wa Kata.
Kauli hiyo imetolewa na wananchi wa Kata hiyo
kawa nyakati tofauti wakati wakiongea na mtandao huu kijijini hapo, ambapo
inadaiwa Mwenyekiti wa Kijiji hicho Bwana John Kalikumoyo ameenguliwa
uongozi kutokana na ubadhilifu pia kuitisha mikutano ya hadhara bila
kibali na kuzuia wananchi katika shughuli za maendeleo.
Wananchi hao wamepinga madai hayo na kuwa ni
njama za mtendaji Kata Bwana Jordan Masweve na Diwani mheshimiwa Alex
Mdimilage, kwani ya kudhoofisha juhudi za mwenyekiti huyo kwa kuzuia mianya ya
upatikanaji wa pesa kinyume na utaratibu wa makusanyo ya pesa za serikali.
Imedaiwa kuwa Viongozi hao wa kata waliitisha
mkutano wa halmashauri ya Kijiji Aprili 17 mwaka huu, wakimtuhumu Bwana
Kalikumoyo kwamba ameuza ng'ombe aliyekamatwa kijijini hapo na kujipatia fedha
jumala ya shilingi milioni 1,080,000 na makosa hayo yanafanya kupoteza sifa za
kuwa kiongozi.
Hata hivyo miongoni mwa vitendo
vinavyolalamikiwa na wanachi kwa viongozi hao ni pamoja na kujipatia zaidi ya
shilingi milioni 24 kutoka kwa wafugaji ambazo hazijaingia katika mfuko wa
kijiji, ba kwamba suala hili Mkuu wa mkoa anapaswa kuunda tume ya kuchunguza
kwani hawapo tayari kuchangia shughuli za maendeleo kama vile ujenzi wa shule
za sekondari, zahanati na maji.
karibuni na kufunguka
milango ya mazungumzo.