ARUSHA: WANANCHI WATAKIWA KUTO WAFICHA WALEMAVU

WA N A N C H I wametakiwa kuacha tabia ya kuwaficha watu wenye ulemavu majumbani wakati wa sensa.

Hayo yamesemwa na Mkuu wa Mkoa wa Arusha, Magesa Mulongo wakati akifungua
warsha ya wadau mbalimbali juu ya kuhamasisha wananchi dhidi ya sensa inayotarajia
kufanyika Agosti 26, mwaka huu.

Mulongo amesema ili kuhesabu watu kutaiwezesha Serikali kurahisisha Mpango wa Maendeleo wa Miaka Mitano na Malengo ya Maendeleo ya Milenia ifikapo 2015 na kuwasihi watu wenye tabia ya kuficha walemavu ili wasihesabiwe, waache mara moja.

Amesema watu wenye ulemavu ni sehemu muhimu kwa jamii hivyo Serikali inataka kujua ni
wangapi ili wawezeshwe na hatimaye kujikwamua kiuchumi na kuondokana na utegemezi kwa
watu mbalimbali.