DAR ES SALAAM: JUBILEE YA MIAKA 75 KUFANYWA NA JUMUIYA YA BRAHIMAKUMARISRAJAYOGA CENTRE

JUMUIYA ya Brahima Kumaris Raja Yoga Centre inayojishughulisha na kutulia na kutafakari
(meditation), itaadhimisha Jubilei ya Miaka 75 kwa kufanya mhadhara kwa umma utakaoendeshwa na bingwa kutoka Urusi, Mtawa Charadhali kesho katika Ukumbi wa Kituo cha Utamaduni cha Urusi, jijini Dar es Salaam.

Mkuu wa Kituo cha Brahma Kumaris Raja Yoga cha Upanga, Sista Dhaerti Patel ameyasema hayo wakati akizungumza na waandishi wa habari kuhusu maadhimisho hayo.

Sista Dhaerti amesema maadhimisho hayo yatahusisha mhadhara wa namna ya kutulia na kutafakari, utakaohutubiwa na bingwa wa fani hiyo, Mtawa Chakradhari kuanzia saa 12 jioni hadi saa 2 usiku katika Ukumbi wa Kituo cha Utamaduni cha Urusi, ambapo hakuna kiingilio.

Ametoa mwito kwa Watanzania wa rangi zote, dini zote, rika zote na jinsia zote kujitokeza kwa wingi ili kufahamu kuhusu kitendo cha kutulia na kutafakari kinavyosaidia kimaisha, na kusisitiza kuwa vitendo hivyo havina dini, bali huwasaidia zaidi watu kuwa karibu kabisa na muumba wao.