WAPIGA DEBE WAWA KERO KWA WASAFIRI


ONGEZEKO la wapiga debe katika vituo vya daladala vya simike na Meta kumesababisha  kuongezeka kwa matukio ya wizi katika vituo hivyo.


Hali hiyo imesababisha abiria wengi kuwalalamikia wapiga debe hao kwa kusema kuwa wengine sio wapiga debe bali wezi wanaokuwa wakiwaibia abiria mizigo yao pamoja na simu, na mikoba hasa ile inayobebwa na wanawake.

Abiria mmoja aliyejitambulisha kwa jina Zawadi Mwasika, begi lake alilokuwa nalo limeibwa pamoja na simu ya mkononi aliyokuwa nayo leo asubuhi wakati akishuka katika kituo cha daladala cha Meta akitokea Mbalizi.

Sanjari na hilo katika kituo cha Simike abiria nao wamekuwa wakilalamikia hali hiyo kwani ongeazeko la wapiga debe katika vituo hivyo vya Simike na Meta umekuwa ukiwapa wasiwasi mkubwa wasafiri na wananchi wanaozunguka maeneo ya vituo hivyo.

Kwa hali hiyo wasafiri wanaotumia vituo hivyo,wanaiomba serikali kuingilia kati hali hiyo kwa kuwaondoa wapiga debe hao au kuwepo kwa ulinzi katika vituo vya daladala.

kwa picha click here