AFYA za Wananchi
zinazidi kuhatarishwa baada ya wafanyabiashara wa Samaki katika ziwa Rukwa
kuanza kutumia dawa za Accaricide zinazotumika katika kuulia wadudu aina
ya Kupe kuhifadhia samaki ili wasiharibike.
Uchunguzi uliofanywa
na MTANZANIA katika maeneo ya Mwambani Wilayani Chunya umebaini kuwa dawa hizo
zimekuwa zikitumika katika kuhifadhia Samaki wabichi ili wasiharibike pindi
wanapowasafirisha tayari kwa ajiri ya kuwauza katika maeneo mengine
nchini.
Mwandishi wa habari
alizungumza na baadhi ya watumiaji wa dawa hizo ambao hawakutaka kutaja majina yao nakueleza kuwa dawa hizo zimekuwa zikiwasaidia sana kuhifadhia samaki
hao licha ya kuchukuwa sikuchache kuishiwa makali.
Mfanyabiashara huyo
alisema wanachokifanya katika matumizi ya dawa hizo ni kwamba wanachukuwa dawa
za kuulia Kupe na kuweka kwenye maji ambayo yanaendana na uwingi wa samaki na
kisha wanaloweka samaki kwa zaidi ya masaa mawili au matatu ambapo alisema dawa
zinakuwa zimeshafanya kazi kwenye samaki katika kuzuia wasiharibike.
Dawa hizo ambazo
zimekuwa zikinunuliwa sana
na wavuvi na wafanyabiashara mikoa ya Rukwa na Mbeya kama anavyoelezea daktari
anayeuza dawa za mifugo jijini Mbeya ambaye hakutaka kutaja jina lake.
Daktari huyo alisema
kwa kuwa ni miaka ya hivi karibuni wafanyabiashara wa dawa hizo waanze
kuzitumia na kudai kuwa licha ya wao kama madaktari kujaribu kuwaeleza madhara
ya dawa hizo lakini bado inashindikana kutokana na wafanyabiashara hao kutumia
kauli ya kwamba wanakwenda kuzitumia katika mifugo yao.
Alisema kuwa suala la
kudhibiti matumizi ya dawa hizo inatakiwa ifanywe na serikali kwa kuanzisha
operesheni ya kupima samaki wabichi kabla hawajaanza kuuzwa kwenye masoko yote
nchini ili kubaini wanaotumia dawa hizo.
IMEANDALIWA NA Michael Mbughi,
KJWA HABARU ZAIDI BONYEZA HAPA