- MPANGO MZIMA KULINDA SIRI ZA WAGOJWA WAO
WAFAMASIA wa nyanda za juu
kusini wametakiwa kuzingatia maadili ya kazi yao na kulinda siri ya mgonjwa na matatizo
yake apotoa huduma.
Rai hiyo imetolewa na mganga
mkuu wa Mkoa wa Mbeya Dr
Bakari Mhina wakati akifungua samina ya siku mbili ya wafamasia wa nyanda za
juu kusini iliyo fanyika mkoani hapa.
Amewataka wafamasia kuwa
makini katika kulinda taaluma yao kwani kazi yao ni kama ya daktari na
wawe wasiri wakati wautoaji wa tiba katika vituo vyao na kuto toa siri za
mgonjwa alizoelezwa.
Mhina amesema wafamasia
wafanye kazi kwa makini na kuzigatia afya ya mgonjwa kwa kumpa dawa sahihi na
maelekezo yanayofaa.