Viongozi wa nchi za Afrika Magharibi , wanachama wa Jumuiya ya kiuchumi ya eneo hilo-ECOWAS,wameuwekea vikwazo vikali uongozi mpya wa kijeshi nchini Mali.
Hatua hiyo imechukuliwa siku moja kabla ya mazungumzo ya dharura ya Umoja wa Mataifa yaliyopangwa kufanyika leo katika taifa hilo ambalo nusu ya ardhi yake inadhibitiwa na waasi wa Kituareg. watuareg hao wameliteka eneo la kaskazini ikiwemo miji miwili mikubwa ya Gabo na Timbuktu. Wakati machafuko yakiendelea nchini humo, tangu watawala hao wa kijeshi waipindue Mali tarehe 22 mwezi Machi, Ufaransa imeliomba Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa kuwa na kikao cha dharura ili kuzungumzia njia za kurejesha amani Mali. Msemaji wa ujumbe wa Marekani katika umoja huo, Mark Kornblau, amethibitisha kufanyika kwa mkutano huo hii leo.