Mapigano makali yamezuka asubuhi ya leo, baina ya vikosi vya serikali ya Syria na waasi, huku utawala wa Rais Basahar al-Assad ukituma askari zaidi katika ngome za waasi hao, licha ya huyo kuahidi atautekeleza mpango wa amani.
.
Shirika la Haki za Binadamu la Syria lenye makao yake mjini London , limesema makabiliano hayo yametokea katika jimbo la kusini la Daraa, kaskazini magharibi mwa jimbo la Idlib na jirani na mji mkuu Damascus. Katika mkoa wa Daraa, mahali lilipoanza vuguvugu la kumpinga Assad, ghasia zilianza usiku wa kuamkia leo katika mji wa Nkhel, baada ya waasi kuvishambulia vituo vya ukaguzi vya kijeshi.
Mwanaharakati mmoja, Sayeed Mahmud ameliambia Shirika la Habari la Ufaransa AFP, kwa njia ya mtandao wa Skype kuwa, nyumba 14 zimechomwa moto na askari hao wanawakamata raia na jeshi limetuma askari wa ziada katika mkoa huo.