MAKATIBU TAWALA WAONYWA


Makatibu tawala hapa nchini wamepewa somo na mkuu wa mkoa Mbeya ABASI   KANDOLO wakati wa ufunguzi wa mkutano wao wa mwaka unaofanyikia mkoani MBEYA ukiongozwa na  Bw GEORGE YAMBESI  kutoka ofisi ya raisi menejimenti ya utumishi wa UMMA

Bw KANDOLO amesema kuwa mkutano huu unatoa fursa kwa ofisi ya raisi menejimenti ya utumishi wa umma  kutoa elimu kwa makatibu tawala wa wilaya kuhusu utendekaji wa kazi na mabadiliko ya kisiasa,kiuchumi,kijamii na kitekinologia nchi na dunia kote.

Hata hivyo  KANDOLO  amesema kuwa kupitia mkutano huo zimewasilishwa maada zinazolenga kuwaelimisha  kuhusu mifumo yna na utatibu mpya  ambazo ni Mbinu za uongozi na majukumu ya katibu tawala wa wilaya ,Wajibu na mjukumu ya makatibu tawala kwenye serikali za mitaa kama watendaji wa kuu,Mafanikio,changamoto na hatuazilizopendekezwa ,kupunguza maambukizi ya ukimwi katika utumishi wa umma.

Pia  amewakumbusha makatibu wa wilaya  kusimamiautekelezaji wa ilani ya uchaguzi wa chama tawala kwa kuzingatia sheria,kanuni,na taratibu zinazowekwa  ili kuhakikisha malengo ya serikali ya kuleta maendeleo ya kijamii,kisiasa,na kiuchumi.