Rais wa Myanmar, Thein Sein amesema kuwa uchaguzi mdogo wa mwishoni mwa juma lililopita , ambapo upinzani ulijizolea viti vingi, ulifanyika kwa mafanikio makubwa.
Jenerali mstaafu huyo ameyasema hayo nchini Cambodia, anakohudhuria mkutano wa Umoja wa viongozi wa Mataifa ya Kusini na Mashariki ya Asia. Chama cha National Laeague for Democracy- NLD kinachoongozwa na mshindi wa tuzo ya amani ya Nobel, Aung San Suu Kyi, kimepata ushindi wa kishindo, mafanikio aliyoyaita ushindi kwa umma, yaliyotokea baada ya miongo kadhaa ya uongozi wa kidikteta; chini ya utawala wa kijeshi.
Chama hicho kilipata viti 40 kati ya 45, matokeo yanayoonekana kuwa pigo kwa Chama tawala, Union Solidarity and Development Party (USDP), kilichoasisiwa na watawala wa kijeshi.
Chama tawala hata hivyo bado kina wingi wa viti kati ya 664 vilivyopo, kutokana na uchaguzi wa bunge 2010 ambapo Bi. Suu Kyi alikuwa kizuizini na chama chake kikaususia uchaguzi huo.