SUNGUSUNGU WANSABABISHIA MWANAKIJIJI KIREMA KWA KUMPIGA NA MARUN

DAUDI Mwashitete (40) Mkazi wa Kitongoji cha Lunyego Kata ya Itaka, Wilaya ya Mbozi Mkoani Mbeya amepata ulemavu baada ya kupingwa na sungusungu wa kijiji hicho, akidaiwa kuwa ni mwizi wa baiskeli.

Majeruhi huyo alikamatwa na sungusungu hao Aprili 8 mwaka 2011 katika Kijiji hicho akiwa na baiskeli yake, akidaiwa kuonyesha risiti ya baiskeli hiyo na yeye kudai kuwa ipo nyumbani kwake ndipo sungusungu hao walipoanza kumpiga kwa marungu yalikuwa yamewekwa misumali kisha kumpiga miguu yote miwili hali iliyompelekea kuvunjika.

Baada ya ukatili huo walimuacha na wao kuondoka na baiskeli yake na zoezi hilo lilisimamiwa na Afisa mtendaji wa kijiji cha Hangomba Bwana Watson Maduguli, ambaye kwa sasa ni Afisa mtendaji wa kijiji cha Bara, Kata ya Bata.

Bwana Mwashitete amepelekwa hospitalini ambapo madaktari walidai akatwe miguu kutokana na kujeruhiwa vibaya miguu hiyo, lakini amekataa na kukimbili kwa Mganga wa Kienyeji ambapo ametibiwa na hivi sasa anaendelea vizuri.