MAONI YATOLEWA SENSA YA WATU NA MAKAZI WAKA HUU WA 2012


 KUFUATIA zoezi zima la sensa ya watu na makazi itakayofanyika Mwezi September  mwaka huu wakazi jijini mbeya wametoa maoni yao mbalimbali kuhusiana na sense hiyo.

Akizungumza na ELIMTAA mwananchi aliyefahamika kwa jina moja la Jakobo amesema kuwa zoezi hili ni la muhimu na pia linaisaidia serikali katika kupanga mikakati ya maendeleo kwa jamii.

Ameongeza kuiwa ili zoezi hili liweze kukamilika serikali inatakiwa kuboresha miundombinu mbalimbali kwa lengo la kuwasaidia watakaokuwa wanafanya kazi ya kuhesabu watu.

Aidha wananchi wameahidi kutoa ushirikiiani wa kutosha kwa serikali na kuweza kutoa taarifa kwa usahihi kwani zitaweza kusaidia katika ugawaji wa huduma za jamii kama elimu na afya.