MWANAJESHI KIZIMBANI KWA MASHITAKA YA KUTOA LUGHA YA MATUSI

ASKARI wa kituo cha jeshi la wananchi Tanzania kilichpo katika mji mdogo wa Mbalizi mkoani hapa, Bw. Chacha Mwita pamoja na raia mmoja  aitwaye Bw. Cosmas Maluli wamepandishwa kizimbani kujibu mashitaka ya kutoa matusi na udhalilishaji  kwa mwenyekiti wa kitongoji  cha Mlima Reli Bw. Ambonisye Ndengelapo Masinga (53).

Imedaiwa mahakamani hapo na Hakimu wa mahakama ya mwanzo Mbalizi Sofia Fungameza kuwa mnamo tarehe 5 na 7 mwezi huu washitakiwa kwa pamoja walitoa kauli za matusi kwa mwenyekiti huyo pamoja na kamati yake,kwamba walikuwa wamehongwa pesa na kununuliwa pombe ili kutoa maamuzi ya kuwatia hatiani washitakiwa hao.

Hata hivyo, waashitakiwa hao walipotakiwa kutoa hoja kuhusiana na tuhuma zinazo wakabili, walikana kwa maelezo kuwa si kweli.

Hakimu amesema washitakiwa wataendelea kuwa chini ya ulinzi mahakamani hapo hadi watu wa kuwawekea dhamana watakapopatikana.

Kesi hiyo iliahirishwa hadi itakapotajwa tena tarehe 24 mwezi huu mahakama mahakamani hapo, Bw. Mwita amepandishwa kizimbani siku moja baada ya kuvamia moja ya  ofisi za waandishi wa habari jijini hapa na kuwatolea vitisho kwamba atawachukulia hatua kufuatia kuandikwa kwake vibaya kwenye magazeti.
Hivi karibuni mnamo tarehe 7 mwezi huu katika eneo la Tazara Mbalizi askari huyo aliwekwa kitimoto na wananchi wa eneo hilo kwa madai kwamba  amekuwa akiwatishia raia hivyo walimtamkia mbele ya afisa  upelelezi wa mkoa wa Mbeya Bw. Elias Mwita kuwa askari huyo ahame uraiani na kumtaka arudi kambini.

Mkuu huyo wa upelelezi alifika kwenye mkutano huo wa hadhara baada ya kufikishiwa malalamiko ofisini kwake kutoka kwa MchungajiBw. Ayub Mwasiposya,Bw.Cosmas Maluli  na Chacha Mwita ambao walipeleka malalamiko yao ofisi za upelelezi  wakimtuhumu Bw.Mwakilembe kuwa ana wanyanyasa wananchi wa eneo hilo.

Malalmiko hayo yalionekana  hayana ukweli baada ya wananchi waliohudhuria mkutano huo kukanusha madai hayo kwa maelezo kwamba hawana matatizo yoyote na Bw. Mwakilembe huku wakimtaka askari huyo ahame makazi yake mtaani hapo kwa sababu walizo zieleza kuwa ni mchochezi na ana tabia ya kutishia raia.

For more chick  here