Bodi ya wafanyakazi wa NSSF wakiwa katika picha ya pamoja baada ya kutoka katika ufunguzi wa mkutano wao uliofanyika katika kumbi za Mbeya Forest Hill Hotel |
- WAHIMIZWA KUWEKA KITEGA UCHUMI
HUDUMA zitolewazo na NSSF zimetakiwa kuboreshwa mara dufu kwa wanachama wake pamoja na familia zao ikikiwa ni pamoja na mafao yao kutolewa mapema wanapo staafu.
Rai hiyo imetolewa na waziri wa kazi na ajira, Gaudentia Kabaka wakati akifungua mkutano wa 38 wa baraza la wafanyakazi wa NSSF uliofanyika mkoani Mbeya, amesema, NSSF inatakiwa kujipanga katika kutoa huduma kwa wanachama wao na familia zao.
Waziri Kabaka amesema atashirikiana na shririka hilo kwa ukaribu kama watamuhitaji kutoa ushirikiano katika kufanikisha mambo yao.
Amesema kumekuwa na matatizo mbalimbali kutoka kwa waajiri ambao wanajua jukumu lao la kupeleka michango yao katika shilika hilo lakini hawafani hivyo na ameutaka mfuko huo kuchukua hatua ya kutunga sheria itakayo wabana waajiri hao.
Kabaka ameutaka uongozi wa NSSF kuhakikisha unatekeleza mradi wa makaa ya mawe wa kiwira mara tu baada ya maamuzi ya serikali kutolewa.
Mbali na mradi huo pia ameushauri uongozi huo kutembelea na kuangalia uwezekano kajika jiji la Mbeya kwani umeme utakapo anza mahityaji yataongezeka kama vile ujenzi wa soko kumbi za mikutano na nyumba za kuishi watumishi.