MWANAJESHI AMUSURIKA KUFA


MWANAJESHI mmoja wa kikosi Karume 44KJ, kilichopo Mbalizi Mbeya, amenusurika kufa baada ya kupata kipigo kikali kutoka kwa wananchi wa eneo la Mbalizi.

Taarifa za uhakika zimeueleza mtandao wa kalulunga kuwa Mwanajeshi huyo pamoja na wenzake siku ya Pasaka walivamia hotel ya Valile na kuanza kutembeza kichapo kwa raia na kuwajeruhi vibaya kisha kutokomea kwa nia ya kurudi kambini ndipo wakakutana na kijana mwingine na kuanza kumpa kipigo.

Baada ya kipigo hicho mwananchi huyo alipiga kelele za mwizi ili kuomba msaada kisha wananchi wakajitokeza na kumkimbiza mwanajeshi huyo kisha kumpa adabu na sasa amelazwa katika Hospitali teule ya wilaya ya Mbeya Vijijini maarufu kama Ifisi.