MUIMBAJI WA NYIMBO ZA INJILI NCHINI APINGWA NONDO.
Mtumishi wa Mungu Bwana Medrick Sanga waimbaji wa Nyimbo za Injili akiwa katika pozi kabla ya kupandishwa jukwaani katika Tamasha la Nyimbo za Injili, sambamba na harambee ya kuchangia fedha za ujenzi wa Kituo cha kulelea Wazee, lililoandaliwa na Bomba FM radio 104.0Mhz Aprili 8 mwaka huu (Sikukuu ya Pasaka) katika Uwanja wa Kumbukumbu ya Sokoine Jijini Mbeya na kudhaminiwa na Kampuni ya SBC Tanzania LTD kupitia kinywaji cha Mountain Dew, Baraka FM, Sweet FM, Generation FM na Rock FM.
Muimbaji wa Nyimbo za Injili nchini kutoka Mkoani Mbeya Bwana Medrick Sanga, mkazi wa Makongorosi, Wilaya ya Chunya amejeruhiwa vibaya kichwani baada ya kuvamiwa na watu zaidi ya saba na kupingwa nondo.
Tukio hilo limetokea Aprili 10 mwaka huu majira ya saa 1:45 usiku alipokuwa anaelekea katika Studio ya kurekodi muziki ya Mbeya (Mbeya Records), zilizopo ndani ya Kanisa la KKKT Usharika wa Forest ya zamani Jijini Mbeya.
Muimbaji huyo amesema alikutana na kundi la vijana wapatao saba na kumtaka asimame nay eye kuwauliza kulikoni, kisha wakaanza kumshambulia kwa nondo na mapanga ambapo alikimbilia barabarani na kuomba msaada wa pikipiki hadi Hospitali ya Mkoa.
Aidha tukio hilo limemsababishia muimbaji huyo wa Injili kuvuja damu nyingi mdomoni ambapo ameng’oka meno kadhaa kutokana na kipigo na kupora simu na pesa.
Medrick ni miongoni mwa waimbaji walioshiriki katika Tamasha la nyimbo za Injili sambamba na harambee ya kuchangia ujenzi wa fesha za ujenzi wa Kituo cha Kulelea wazee, lililofanyika Aprili 8 mwaka huu katika Uwanja wa Kumbukumbu ya Sokoine lililoandaliwa na Kituo cha kutushia matangazo Bomba FM redio cha mkoani hapa.
Hata hivyo muimbaji huyo ambaye ni kivutio cha mashabiki awapo jukwaani amefanyiwa vipimo vya uchunguzi (X-RAY), ambapo hali yake kwa sasa inaendelea vema.