Picha hizi zilipigwa tukiwa njiani kurudi campsite baada ya kumaliza mizunguko (game drive) ndani ya pori la akiba la Selous. Ukiwa unatoka kuelekea Kijijini (Mloka) utapita mahali ambapo ndio mpaka wa game reserve na eneo la kijiji.
Hii
sio njia inayotumiwa na wageni bali ni njia ambayo inatumiwa na
wahifadhi kufanya ukaguzi wa mipaka ya hifadhi. Kimsingi, barabara hii
ni sehemu/alama ya mpaka wa pori la akiba. Upande wa kulia wa Barabara
ni Pori la Akiba wakati upande wa kushoto wa barabara ni eneo la Kijiji
cha Mloka.
Hifadhi hii inapatikana mkoani Morogoro ila vijijini hapa Tanzania