Uncategories
KILICHOMUUA HASA MSANII WETU MPENDWA NI :
KILICHOMUUA HASA MSANII WETU MPENDWA NI :
baada ya jopo la madaktari bingwa watano wa Hospitali ya Taifa
Muhimbili kuufanyia uchunguzi mwili wa marehemu huyo, zimeeleza kuwa
tatizo hilo linaweza kumfanya mtu apoteze maisha mara moja au baada ya
siku kadhaa. Mmoja wa madaktari hao ambaye aliomba jina lake lisitajwe
gazetini alisema waligundua tatizo hilo baada ya kumfanyia uchunguzi huo
kwa zaidi ya saa mbili. “Tulianza kuufanyia uchunguzi mwili wa marehemu
kuanzia saa 4:00 asubuhi hadi saa 6:45 mchana na tukagundua kuwa
marehemu alifariki kutokana na mtikisiko wa ubongo kwa kitaalamu, Brain
Concussion,” alisema daktari huyo. Alisema Kanumba alipata mtikisiko wa
ubongo ambao husababisha kufeli kwa mfumo wa upumuaji
(cardio-respiratory failure) “Kilichomuua hasa ni mtikisiko wa ubongo,
ambao endapo unatokea katika sehemu ya nyuma ya ubongo (cerebrum), huua
kwa haraka” alisema daktari huyo na kuongeza kuwa mtikisiko wa ubongo wa
nyuma, husababisha matatizo ya mfumo wa upumuaji na hilo limeonekana
katika mwili wake. “Baada ya ubongo wake kutikiswa kwa nguvu, mfumo wa
upumuaji ulifeli na ndiyo maana tumekuta kucha za Kanumba zikiwa na
rangi ya bluu, huku mapafu yake yakiwa yamevilia damu na kubadilika kuwa
kama maini, hizo ndizo dalili za kufeli kwa mfumo wa upumuaji.