Picha
hizi zilipigwa tukiwa njiani kurudi campsite baada ya kumaliza
mizunguko (game drive) ndani ya pori la akiba la Selous. Ukiwa unatoka
kuelekea Kijijini (Mloka) utapita mahali ambapo ndio mpaka wa game
reserve na eneo la kijiji.
Hii
sio njia inayotumiwa na wageni bali ni njia ambayo inatumiwa na
wahifadhi kufanya ukaguzi wa mipaka ya hifadhi. Kimsingi, barabara hii
ni sehemu/alama ya mpaka wa pori la akiba. Upande wa kulia wa Barabara
ni Pori la Akiba wakati upande wa kushoto wa barabara ni eneo la Kijiji
cha Mloka.
KWA PICHA ZAIDI BOFYA HAPA