POLISI mkoani Lindi imewafukuza kazi askari wake wawili kati ya 24 waliotuhumiwa kwenda kinyume cha maadili ya jeshi hilo kwa kipindi cha mwaka mmoja uliopita.
Kaimu Kamanda wa Polisi wa Mkoa, George Mwakajinga, amewaeleza waandishi wa habari, juu ya hatua zinazochukuliwa na jeshi hilo katika kuhakikisha linadumisha maadili.
Mwakajinga amesema askari hao wawili waliofukuzwa kazi, wote ni wanaume na walifukuzwa kati ya Machi 2011 hadi Machi mwaka huu.
Kaimu Kamanda huyo amefafanua kwamba katika kipindi cha kuanzia Machi 2011 hadi Machi mwaka huu, askari Polisi wapatao 24 wa vyeo mbalimbali, wameshitakiwa kijeshi na kuadhibiwa, kati ya hao wawili ndiyo waliotimuliwa kazi.
Mwakajinga ameeleza katika kutunuku Tuzo hizo zilizojumuisha wilaya zote tano za mkoa huo, watu 29 wakiwamo askari 24 kati yao 17 wanaume na saba wanawake na wadau watano akiwamo Meneja wa Benki ya CRDB Tawi la Lindi, Afwilile Mbembelwa, wametunukiwa Tuzo na Hati ya Kamanda wa Polisi Mkoa.
Pia amesema Tuzo hizo zimetolewa kwa kuangalia nidhamu, juhudi mbalimbali kazini, uadilifu na ushirikiano na wadau ndani na nje ya Jeshi hilo ambapo kila mmoja alipata cheti na fedha taslimu kiasi cha Shilingi elfu hamsini.
kwa habari zaidi BOFYA HAPA